×

Quick Rocka, Msami Watoa Shavu kwa Washindi wa Promosheni ya Kubwa ya Moto

Kampuni ya simu za mkononi ya lnfinix Tanzania imekamilisha rasmi promosheni ya #Kubwayamoto ambayo ilikuwa ikifanyika katika kipindi cha Sikukuu za Christmas na Mwaka mpya.

Mabalozi wa lnfinix HOT 40 Pro, @quickrocka na @msamibaby walikabidhi zawadi ya skuta kwa mshindi, Karimu pamoja na laptop mbili kwa Eric Briton na Faridhma ambao waliibuka na ushindi kati ya wateja wote ambao walifanya manunuzi katika kipindi hicho, huku wateja wengine wakijishindia
lnfinix HOT 40 Pro, simu ambayo ilizinduliwa Desemba 2023 jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia ushindi wa skuta, mshindi Karim alisema:
“Nimefurahi sana kuibuka mshindi, kwa kweli mwaka 2024 umeanza vizuri kwangu na familia yangu, mimi ni mwanafamilia wa lnfinix tangu Note 7 hadi sasa namiliki lnfinix ZERO 30 5G nimekuwa nikifurahishwa na namna simu zao zinavyodumu na chaji, kufungua applications kwa haraka lakini kubwa zaidi bei sio za kuumiza.”


Vilevile @infinixmobiletz imetoa shukrani kwa wateja wa simu zao kwa ushirikiano ambao wameuonyesha kwa 2023 lakini pia imeahidi kuja na matoleo yenye teknolojia ya kuendana na mwaka huu wa 2024.

Promosheni ya Kubwa ya Moto ilikuwa ikifanyika kwa mikoa yote yenye bidhaa za lnfinix, simu ambazo zilikuwa katika promosheni hiyo ni Zero 30, NOTE 30 Series, HOT 30 Series na HOT 40 series.

#kubwayamoto

Leave a Comment