KOCHA Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha ametamba kuwa ataingia kivingine kwa kufanya mabadiliko ya kikosi cha timu hiyo katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) dhidi ya Tembo utakaochezwa kesho Jumatano katika Uwanja wa Azam Complex.
Mabadiliko hayo ni baada ya baadhi ya nyota wake walikuwa kwenye majukumu ya timu zao za taifa ikiwemo Tanzania ambao ni Aishi Manula, Mohammed Hussein, Mzamiru Yassin na Kibu Denis, Zambia akiwa Clatous Chama ambao wanatarajiwa kujiunga na timu yao kuanzia leo baada ya kuondolewa katika hatua ya makundi ya fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON).
Akizungumza na Championi Jumatatu, Benchikha alisema anategemea kufanya mabadiliko ya kikosi kuelekea katika mchezo wao ujao wa FA dhidi ya Tembo ambao utamsaidia kuandaa kikosi chake rasmi kwa ajili ya michezo iliyopo mbele yao ikiwa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Alisema licha ya kutokuwepo kwa nyota muhimu ambao wako kwenye majukumu ya timu za taifa na wengine kujiunga hivi karibuni baada ya kuondolewa lakini haitaathiri mipango ya mbinu zake kuelekea mchezo huo wa ASFC.
“Kuna baadhi ya wachezaji hawakuwepo kwenye maandalizi ya mechi yetu ijayo, tulianza nao wanajua umuhimu wa mchezo huo, mabadiliko yatakuwepo madogo kwa sababu kuwapa nafasi nyota wapya lakini tukichanganya na wale waliopo mwazo.
“Ninapambana kwa moyo wote kwa ajili ya kushinda kila siku, Simba tupo kwenye michuano ya CAF ambao nataka tufike mbali zaidi ya matarajio ya wengi, lakini ubingwa wa ligi ni muhimu lazina tufanye vizuri tushinde,” alisema kocha huyo.
Aliongeza kuwa yupo Simba kuendelea kufanya kazi yangu kwa jitihada zote kuhakikisha wanaendeleza furaha kwa mashabiki wao na kufikia kile ambacho kinatararajiwa na wanasimba katika kila mechi zilizopo mbele yao.
KOCHA Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha ametamba kuwa ataingia kivingine kwa kufanya mabadiliko ya kikosi cha timu hiyo katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) dhidi ya Tembo utakaochezwa keshokutwa Jumatano katika Uwanja wa Azam Complex.