×

Benchikha Azitolea Macho Dakika 180 dhidi Mashujaa FC

KOCHA Msaidizi wa Simba, Seleman Matola ameweka wazi kuwa kwa sasa hesabu zao wanazopiga ni kuhakikisha wanafanikiwa kivuna pointi sita katika mechi mbili za kanda ya magharibi.

Kikosi cha Simba kimeondoka jana asubuhi kuelekea Kigoma na tayari kwa mchezo wa kiporo dhidi Mashujaa FC utakaochezwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika baada ya hapo wataenda Tabora kucheza na Tabora United Februari 6, mwaka huu Uwanja wa Al Hassan Mwinyi.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Matola alisema wameona mapungufu baada ya mechi yao na Tembo FC waliyoshinda 4-0 juzi ikiwa ya Kombe la FA hivyo sasa nguvu wanaielekeza kwenye michezo miwili ya ukanda wa Magharibi ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri na kurejea na ushindi.

“Mechi yetu inayofuata dhidi ya Mashujaa FC ni mechi ngumu na uwanja wake mgumu lakini tumejipanga kwa ajili ya kupata ushindi.

“Tunachokiangalia kama benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha ni kuangalia namna gani tunaweza kufikia malengo ya kuhakikisha tunaweza kupata matokeo katika michezo yote miwili kutokana nafasi ambayo tupo kwa sasa,” alisema Matola.

Stori Na Ibrahim Mussa

NAJUA HILI HULIFAHAMU KUHUSU RAPA KUTOKA MAREKANI ANAYEENDA kwa JINA LA 21SAVAGE BASI NGOJA NIKUJUZE

Leave a Comment