×

Mkurugenzi Wa Mawasiliano Ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus Azungumza Na Wahariri – (Video+Video)


Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus pamoja na Viongozi wengine wakizungumza na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu ziara za Rais Samia Suluhu Hassan alizozifanya Vatican, Norway na Ethiopia, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo tarehe 22 Februari 2024.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kuwa upungufu wa sukari umesababishwa na uzalishaji mdogo wa zao la miwa.

Akizungumza katika mkutano wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu na wahariri wa vyombo vya habari, Bashe amesema hali ya kilimo cha miwa ni mbaya na imesababisha uzalishaji wa zao hilo kushuka hivyo kusababisha upungufu wa sukari.

“Mpaka sasa sukari iliyopo bandarini na ambayo imeshaanza kusambazwa ni tani elfu 31, Hivi sasa tunavyoongea kuna meli ya zaidi ya tani 25,000 inashusha sukari.”

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari, 2024.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari 2024.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Mohamed Bashe akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari, 2024
Baadhi ya Wahariri na Waandishi kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi Ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari, 2024.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba Katibu Mkuu akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari, 2024
Balozi Shaibu Said Musa – Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari, 2024.

Leave a Comment