
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso ametoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya Maji inayotokana na chanzo cha Ziwa Victoria ikiwa ni kazi ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kujibu ajenda na hoja za Wabunge wa Mkoa wa Mara.
Waziri Aweso ameeleza hayo akiwa katika ziara ya Mhe Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye mkutano wa wanachi mji wa Utegi wilayani Rorya Mkoa wa Mara.
Akifafanua mbele ya wananchi wa Rorya na Waziri Mkuu, Aweso Ameeleza kuwa kwa wilaya za Rorya na Tarime upo Mradi mkubwa wa kiasi cha Bilion 134, Kwa Musoma Mjini mradi wa Bilion 46.
Pia, Waziri wa Maji ameeleza kwa Upande wa Musoma vijijiji Kuanzia Mugango hadi Kiabari na Butiama upo mradi wa Bilion 70.5 na Wilaya ya Bunda kiasi cha Bilion 10.6.
Waziri ameeleza kwamba hii ni ile miradi mikubwa na kwamba ipo mingine ya kati na midogo mingi sana ambayo chanzo chake ni ziwa Victoria katika wilaya zote za Mkoa wa Mara.