×

Makamu Wa Rais Akiongoza Waombolezaji Kuaga Mwili Wa Hayati Ali Hassan Mwinyi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam. Tarehe 01 Machi 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimfariji Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati wa kuaga mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam. Tarehe 01 Machi 2024.

Mwili wa Rais na Amiri Jeshi Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi leo umeagwa katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar ambapo mwili uliingizwa na msafara uliingozwa kijeshi ukisindikizwa na vifaru vya kivita.

Leave a Comment