Rais wa Zanzibar Ajumuika na maelfu ya wananchi na viongozi mbalimbali katika Maziko hayati Ali Hassan Mwinyi, Zanzibar (Picha +Video)
Global Publishers March 3, 2024 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la baba yake, Rais mstaafu, hayati Ali Hassan Mwinyi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj. Dk. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na maelfu ya wananchi na viongozi mbalimbali katika Dua, Sala na Maziko ya aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassani Mwinyi yaliyofanyika Machi 2, 2024 Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Maziko ya Ali Hassan Mwinyi yamefanyika kwa taratibu za dini yake ya Kiislamu na kiserikali, kama viongozi wengine wa kiserikali wanavyozikwa.
Rais mwinyi amezikwa kijiji cha Mangapwani Zanzibar mahali alipokulia na kusoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiweka mchanga katika kaburi la Rais mstaafu, hayati Ali Hassan Mwinyi.Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Abdulrahman Kinana akiweka mchanga katika kaburi la Rais mstaafu, hayati Ali Hassan Mwinyi. Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, akiweka mchanga kwenye kaburi, wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mstaafu na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Pili, Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi.…Maziko ya Rais mstaafu, hayati Ali Hassan Mwinyi yakiendelea.… Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi wakati wa maziko ya baba yake yakiendelea.…Dua, Sala na Maziko ya aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassani Mwinyi.Kaburi ulimohifadhiwa mwili wa Rais mstaafu wa Tanzania, hayati Ali Hassan Mwinyi.Wanajeshi wakiwa wamebeba mwili wa mwili wa Rais mstaafu wa Tanzania, hayati Ali Hassan Mwinyiwakati wakielekea kwenye maziko Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja.Bibi Siti Mwinyi Mjane wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi na Familia yake wakiwa katika Simanzi na majonzi wakati Jeneza lenye mwili wa Hayati Mzee Mwinyi likitolewa mara baada ya kuswaliwa kuelekea kwenye Makaburi kwa ajili ya Maziko yaliyofanyika Kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 02 Machi 2024.Rais Samia pamoja na Viongozi wengine mbalimbali wakiomba Dua ya pamoja kabla ya maziko ya Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi.Viongozi Wastaafu mbalimbali wakiwa katika kisomo na Dua kabla ya mazishi ya Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi yaliyofanyika Kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 02 Machi 2024.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi akishindwa kujizuia kwa huzuni wakati wa shughuli za kuaga mwili wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar tarehe 02 Machi 2024.Ndugu na Jamaa wakiwa ndani ya majonzi makubwa wakati wa shughuli za kuaga mwili wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar tarehe 02 Machi 2024.