×

Waziri January Makamba Akanusha Taarifa za EAC Kutambulisha Noti Mpya

Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika mashariki, January Makamba.

Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika mashariki, Mhe. January Makamba amekanusha taarifa zilizosambaa kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kwa mara ya kwanza imetambulisha noti yake itakayotumika katika nchi wanachama, iliyopewa jina la SHEAFRA (SHF).

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii Mhe. Makamba amesema “Hizi taarifa si za kweli.”

“Taratibu na vigezo vya kiuchumi na kitaasisi vya kufikiwa kwa Umoja wa Fedha (Monetary Union)/Sarafu Moja (Single Currency) kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki bado kukamilika. Mapendekezo ni kufika hatua hiyo mwaka 2031.”—Mhe. Makamba.

Leave a Comment