
Legal Services Facility (LSF) na Enabel, shirika la maendeleo la Ubelgiji, wamesaini rasmi mkataba wa ruzuku wa bilioni 10.7 za Kitanzania leo kutekeleza Maboresho ya Upatikanaji wa Haki kwa Wanawake kupitia Msaada wa Kisheria.
Mradi huu shirikishi unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya chini ya mradi unaoitwa "Gender Transformative Action: Breaking the Glass Ceiling" na unalenga kupunguza unyanyasaji wa kijinsia na kuongeza usawa katika upatikanaji wa haki hususani kwa wanawake na wasichana.

Chini ya makubaliano hayo LSF na Enabel zitashirikiana kuwekamazingira wezeshi na mazuri ya upatikanaji wa haki kwa kujenga uwezo wa wasaidizi wa kisheria na watoa msaada wa kisheria kuweza kutoa huduma bora za msaada wa sheria.
Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng'wanakilala amesema "Kupitia mradi huu, LSF itahakikisha kuwa huduma za msaada wa kisheria zenye ubora zinapatikana kwa watu wote kupitia mifumo rasmi na isiyo rasmi ya utoaji haki. Lulu amefafanua zaidi kuwa mradi huu utaongeza uelewa wa jamii hususani wanawake na wasichana kuhusina na umhimu wa msaada wa kisheria katika.
” Tuna furaha kutia saini mkataba huu na Enabel, kwa kuwa umelenga katika kufikia malengo na hatua zote muhimu katika
kuboresha upatikanaji wa haki kupitia huduma za msaada wa kisheria hasa kwa wanawake, wasichana,
na jamii zote zilizopo nchini Tanzania.

Mwakilishi Mkazi wa Enabel nchini Tanzania, Koenraad Goekint, alisema, "Tunafurahi kuanzisha ushirikiano huu muhimu na Kituo cha Huduma za Kisheria (LSF) wenye nia ya kuimarisha upatikanaji wa haki, hasa kwa wanawake, wasichana, na jamii zilizotengwa nchini Tanzania.
Ushirikiano huu unathibitisha dhamira yetu ya kukuza maendeleo endelevu na kujenga jamii iliyo na usawakatika upatakanaji wa haki na inayoshiriki kikamilifu katika mfumo wa sheria.
Naye Balozi Christine Grau – Balozi wa Jumuiya ya Ulaya Nchini Tanzania na Afrika Mashariki., katika hotuba yake amesema kupitia mradi huu EU inaendelea kushirikiana na wadau katika kuongeza upatikanaji wa haki kwa wanawake na wasichana hasa wale amabo ni whanga wa ukatili wa unyanyasaji wa kijinsia “Kwa hakika mradi huu unaenda sambamba na juhudi zingine zenye nia ya kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuongeza ushiriki wao katika uongozi na uwakilishi wao katika vyombo vya
maamuzi.
Kuhusu LSF.
Legal Services Facility (LSF) ni shirika lisilo la kiserikali linaloongoza katika kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wote, hasa kwa wanawake kupitia uwezeshwaji wa kisheria. Tangu Kuanzishwa kwake mwaka 2011, LSF imejikita katika kuwezesha upatikanaji wa haki nchini ikiwemo kuboresha upatikanaji wa huduma bora za msaada wa kisheria kupitia zaidi ya ya watoa huduma za msaada wa kisheria takribani 4000 na mashirika ya msaada wa kisheria 200 nchini Tanzania Bara na Zanzibar.
Katika kutekeleza shughuli zake , LSF hufanya utekelezaji moja kwa moja wa programu zake pamoja na kutoa ruzuku kwa mashirika
yanayotoa huduma za msaada wa kisheria,na kutekeleza programu za kuwawezesha wanawake kiuchumi, haki za jinai, suluhu mbadala za migogoro (ADR) , na programu ya upatikanaji wa haki kwa ujumla. LSF hufanya kazi kwa karibu na serikali katika ngazi zote, wadau wa maendeleo,sekta binafsi, mashirika ya Umoja wa Mataifa, na wadau wengine nje ya kanda ili kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wote hususani kwa wanawake ,wasichana, watu wenye ulemavu, na makundi yaliyosahaulika
Kuhusu Enabel:
Enabel ni shirika la maendeleo la Ubelgiji lenye dhamira ya kujenga jamii endelevu, inayoishi katika hali ya usawa, haki. Kwa kipindi cha mwaka 2020 -2030 Shirika la Enabel limeweka kipaumbele katika kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya Tabianchi, amani na usalama Pamoja na maswala ya haki na usawa.
Shirika la Enabel lina uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta za elimu, afya, kilimo, utunzaji wa mazingira, TEHAMA, ajira, na utawala bora. Katika kutekeleza shughuli zake kwa nia ya kufikia malengo yake, Shirika la Enabel linashirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo serikali ya Ubelgiji, Umoja wa Ulaya, serikali za nchi husika, sekta binafsi pamoja na jamii yote kwa ujumla.
Kuhusu “Gender Transformative Action: Breaking the Glass Ceiling”: Programu ya "Gender Transformative Action: Breaking the Glass Ceiling" ni mpango uliofadhiliwa na Umoja wa Ulaya wenye thamani ya jumla ya euro milioni 90, ukiwa na lengo la kuharakisha maendeleo kuelekea usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake nchini Tanzania. Ikiwa na vipengele vitatu kuu –
i) Kuwezesha mazingira na sera za usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake, ii) Uwezeshaji wa Kiuchumi wa Wanawake, na iii) Uongozi, ushiriki, na haki – Programu hutekelezwa kwa ushirikiano na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto – kama kiongozi wa Sera ya Kitaifa ya Jinsia na Maendeleo – pamoja na wizara muhimu kama vile Sheria, Elimu, na Afya.
Wizara ya Fedha hupokea msaada wa bajeti ambao huelekezwa kwa wizara zinazotekeleza sera muhimu. Washirika wanaotekeleza
vipengele vingine ni pamoja na LSF, TASAF, Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, na benki za biashara za Kitanzania zinazotoa ufikiaji wa fedha; taasisi ya UONGOZI na mashirika ya kiraia pia wanashiriki.
Programu hutekelezwa pia kwa ushirikiano na wadau mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa, ENABEL, SIDA, Ushirikiano wa Kifini na Kijerumani, na Benki ya Dunia, kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali na kuzidiana.