×

Siku ya Wanawake Duniani Buchosa Wamfariji Mtoto Mlemavu

Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 8 ya mwezi wa tatu ambapo wanawake hukutana katika maeneo mbalimbali kujadili changamoto na mafanikio yao.
Wanawake wa halmashauri ya buchosa wao maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani machi 6 mwaka huu katika kata ya Nyakasasa iliyopo katika kiziwa cha kome wilaya ya sengerema mkoani mwanza.
Maadhimisho hayo yameongozwa na mkuu wa wilaya ya sengerema Senyi Ngaga yakiwa na kauli mbiu ya wekeza kwa wanawake kuharakisha maendeleo ya taifa na ustawi wa jamii.
Wakisoma risala yao kwa mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo wanawake wa halmashauri ya buchosa walimuomba kuongoza wanawake wengine ili waweze kumsaidia mtoto Dotto Sabila ili aweze kupata fedha na mahitaji yake ya kuendelea na masomo.
Mtoto Dotto alifaulu kujiunga na kidato cha kwanza shule ya sekondari mwanza girl mwaka Jana lakini mazingira ya shule yalimfanya ashindwe kusoma kutokana na miundombinu kutokuwa rafiki kwake na familia yake kuwa duni hivyo kuhitaji msaada wa watu ili aweze kutimiza ndoto zake za kupata elimu.
Katika zoezi hilo zaidi ya shilingi laki mbili zilipatikana kutoka kwa wanawake wa halmashauri ya buchosa ikiwa ni utamaduni wao wa kusaidia watu wasiojiweze kwenye maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani hivyo binti Dotto bado anahitaji msaada ili kupata haki yake ya msingi ya kupata elimu.
Pamoja na mambo mengi wanawake wa halmashauri ya buchosa wameiomba serikali mambo kadhaa ambayo yatawasaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja,Jamii ya wanabuchosa na taifa kwa ujumla.
Baadhi ya mambo waliyoyaomba ni pamoja na kuwezeshwa kwa kupewa mikopo,kupatiwa elimu ya ujasiriamali, kupewa nafasi za uongozi kwenye gazi mbalimbali, kupatikana kwa madaktari na wauguzi kwenye zahanati,vituo vya afya na hospital za halmashauri hiyo.
Aidha wameomba kuletewa kivuko kikubwa ambacho kitasaidia kwani kilichopo hakitoshi kulingana na idadi kubwa ya watu wanaoishi kisiwani kome na shughuli mbalimbali zinazofanyika katika kisiwa hicho.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo Senyi Ngaga amesema serikali ilijitahidi kuhakikisha wanawake na jamii kwa ujumla inafanya shughuli za kuinua uchumi kwa serikali kutegeneza miundombinu wezeshe ikiwemo shule,barabara,maji,umeme,kilimo na mambo mengine mengi yanayofanya na serikali chini ya rais Samia.
Aidha Senyi amewataka wanawake wa halmashauri ya buchosa kujitokeza kwa wingi kuomba nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani kwani kufanya hivyo kutasaidia kuondoa unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake.

Leave a Comment