×

Serikali Ya Mtaa Tandika Mabatini Yaitisha Mkutano Wa Hadhara Kueleza Ilivyotimiza Ilani Ya CCM

Mwenyekiti Shariff Mustafa Jumbe akieleza jinsi mtaa wake ulivyotekeleza ilani ya CCM

Dar es Salaam 9 Machi 2024: Serikali ya Mtaa wa Tandika Mabatini jijini Dar inaMt yoongozwa na Mwenyekiti Shariff Mustafa Jumbe na wajumbe, wake wote kutoka Chama cha Mapinduzi, leo imefanya mkutano wa hadhara mtaani hapo kwa ajili ya kueleza jinsi ilivyotekeleza ilani ya chama hicho kama ilivyowaahidi wananchi wakati wakiingia madarakani kwenye uchaguzi uliopita.

Mgeni rasmi katika mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke, Mh. ZenaYusuf Mgaya mwenye miwani katikati akiwa na wageni wengine.

Katika mkutano huo Shariff alieleza jinsi yeye na wajumbe wake walivyotekeleza ahadi mbalimbali walizowahidi wananchi kama vile kuboresha huduma za afya, elimu, ulinzi, miundombinu na usalama wa raia.

Shamrashamra zilivyokuwa.

Wananchi waliofuriika kwenye mkutano huo walionekana kumshangilia Mwenyekiti huyo huku wengine wakipiga mayowe na kusikika wakisema “Shariff mitano tenaaa…”

HABARI/PICHA NA ISSA MNALLY WA GPL

Leave a Comment