×

Alichokisema Kadogosa Uzinduzi wa Safari ya Kwanza ya SGR- Dodoma

Safari ya Kwanza ya majaribio ya Treni ya SGR kutoka Dar-es-Salaam mpaka Dodoma Katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60, ya Muungano wa Tanzania mafanikio ya Serikali ni mradi wa ujenzi wa reli ya kiwango Cha kimataifa yaani SGR unatekelezwa katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ni kutoka Dar-es-Salaam hadi Mwanza, na awamu ya pili ni kutoka Tabora Hadi Kigoma

Hayo yamezungumzwa Leo Aprili 21, 2024, na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa wakati wa Uzinduzi wa safari ya kwanza ya majaribio kutoka Dar-es-Salaam mpaka Dodoma ikiwa ni maagizo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwamba mpaka kufikia mwezi Julai Treni hiyo iwe imeanza kufanya safari kutoka Dar-es-Salaam mpaka Dodoma.

Amesema pamoja na uendeshaji na kuendeleza miundombinu ya reli Shirika la Reli (TRC) linaendelea na usimamizi wa mradi huo wa SGR ambao ni Mmoja wa miradi mikubwa Nchini Tanzania wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 10.016 ni sawa na fedha za Kitanzania trilioni 23.3

“Ujenzi unatekelekezwa kwa vipande vitano kwa maana ya awamu ya kwanza kutoka Dar-es-Salaam mpaka Morogoro, ambao kwa asilimia 98.93, kipande hicho kimeshaisha sehemu kubwa ambayo tunajenga Sasa hivi ni kuingia bandarini, lakini Kuna pale Vingunguti, Airport amesema Kadogosa.

Na Neema Adrian

Leave a Comment