
Watoto wawili wa familia moja katika Mtaa wa Mindu mkoani Morogoro, wamefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye shimo lenye maji linalodhaniwa kuwa ni la choo ambalo lilikuwa halijaanza kutumika, tukio lililotokea Aprili 23, mwaka huu wa 2024.
Watoto hao ni Neema Emmanuel (11) mwanafunzi wa darasa la nne na Glory Geitan (12) anayesoma darasa la tano.
Jeshi la zimamoto na uokoaji limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema miili ya watoto hao tayari imetolewa katika shimo hilo na imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.