×

Ally Hapi Awataka viongozi Chama na Jumuiya zake Kudhibiti watendaji wa Serikali Wanaotoka Kwenye Misingi

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ally Hapi amewataka viongozi Chama na Jumuiya zake Kudhibiti watendaji wa Serikali wanaotoka kwenye misingi na maadili ya kazi zao, na kuwa wa kwanza kutoa taarifa za kukemea zinapotokea changamoto mbalimbali.
Ali Hapi ametoa maelekezo hayo akiwa Kata ya Nyang’olo Iringa Vijijini, Wilaya ya Iringa Tarafa ya Isimani alipokuwa akizungumza na Wananchi na wanachama wa Chama hicho katika ziara yake ya siku tatu aliyoianza Leo mkoani humo.
“Msikae na kuzunguka na mashati yakijani tu, ukiona Mtendaji wa Kata hatendi haki, Mwenyekiti wa CCM Kata unayo nafasi ya kumuita kwenye ofisi yako ukamuuliza, na CCM itapendwa na kuaminiwa, Watendaji miungu watu na wanaoonea watu , lazima CCM tushughulike nao, tunataka Dkt. Samia akija akipita hapa watendaji wanaomsaidia wawe wameshafanya kazi vizuri na asiwe na deni Kwa Wananchi, masuala ya wafugaji, wakulima na kero ndogo ndogo zifanyiwe kazi,” amesema Ally Hapi

Leave a Comment