×

Helikopta Iliyombeba Rais wa Iran Yapata Ajali, Juhudi za Kuitafuta Zapamba Moto

Helikopta iliyokuwa imembeba Rais wa Iran, Ebrahim Raisi imeripotiwa kupata ajali leo Jumapili, Mei 19, 2024 Mashariki mwa Azerbaijan.

Shirika la habari la Tehran Post limeeleza kwamba Rais Raisi alikuwa na watu wengine watatu kwenye helikopta hiyo ambao ni Ayatollah Al-Hashem, kiongozi wa dini kutoka Tabriz, Hossein Amir Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje na Malek Rahmati, Gavana wa Jimbo la Azerbaijan Mashariki.

Taarifa zinazidi kueleza kuwa Rais Raisi alikuwa kwenye msafara wa helikopta tatu ambapo mbili zilitua salama huku aliyokuwa amepanda yeye ikipata ajali.

Tayari vikosi vya uokoaji vimefika eneo la tukio na juhudi za kuitafuta helikopta hiyo zinaendelea huku hali ya ukungu mwingi ikisababisha ugumu.

Inaelezwa kwamba simu ya satelite anayoitumia rais huyo kwa ajili ya usalama, bado haionekani na kusababisha iwe vigumu kujua ni wapi helikopta hiyo ilipoangukia.

Leave a Comment