
Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imempitisha Khamis Yussuf Mussa (Pele) kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mdogo wa Kwahani.
Pia kamati hiyo, kwa niaba ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) imefanya uteuzi wa Suzan Kunambi, kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), nafasi iliyoachwa wazi na Jokate Mwegelo, aliyeteuliwa kuwa Katibu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Taifa.

Kabla ya uteuzi huo, Suzan alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Mjini Magharib Zanzibar.
Uteuzi huo umefanywa na Kamati Kuu iliyoketi Makao Mkuu ya CCM Kisiwandui, Zanzibar Mei 19, 2024 chini ya Makamu Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi.
Akitoa taarifa ya kikao hicho, Katibu wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na, Uenezi na mafunzo, Amos Makalla amesema Kamati Kuu imeona Yussuf ndiye anayetosha kupeperusha bendera hiyo.
Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Juni 8, 2024, unafanyika baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Ahmed Yahya Abdulwakil kilichotokea Aprili 8 mwaka huu, kutokana na shinikizo la damu.
