
Abiria mmoja amefariki na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa kwenye ndege ya shirika la ndege la Singapore kutoka London kuelekea Singapore kukumbwa na msukosuko mkubwa.
Ndege hiyo aina ya Boeing 777-300ER iliyokuwa inaenda Singapore ilielekezwa Bangkok na kutua saa kumi kasoro robo kwa saa za ndani (08:00 GMT).
Ndege hiyo ilikuwa na jumla ya abiria 211 na wafanyakazi 18, shirika hilo la ndege lilisema katika taarifa yake.
“Singapore Airlines inatoa rambirambi zake za dhati kwa familia ya marehemu,” ilisema.