
ALIYEKUWA mume wa msanii wa Bongo Muvi na mjasiriamali anayemiliki mgahawa maarufu wa Shishi Food, Zuwena Mohamed almaarufu Shilole aitwaye Rommy leo Mei 28, 2024 amethibitisha kuachana na staa huyo.
Hii ni baada ya hivi karibuni Shilole kuonekana kwenye mitandao ya kijamii akifurahia maisha na mwanaume mwingine, huku mashabiki wa Shilole wakiwa katika pande mbili tofauti wengine wakimpongeza na wengine wakichukizwa na tabia ya msanii huyo kubadilisha wanaume kila mara.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rommy 3D amethibitisha kuacha na msanii huyo:
“Habari…..Ndugu zangu kama ambavyo mmeona kwenye mitandaoni na hiyo ndio hali halisi basi Mimi na aliyekuwa mwenzangu Zuwena Mohamed (Shilole). Naona tumefikia Mwisho na si Vibaya nikakubali matokeo na kumpisha Kijana mwenzangu aendeleze gurudumu hili, na Maisha yaendelee… nipende kutoa shukrani zangu za dhati kwa vile tulivyoishi siku zote za mapenzi yetu.
Wabillah Tawfiq” ameandika Rommy ambaye hakujaaliwa kupata mtoto na Shilole katika ndoa yao.

(STORI NA NICOLAUS TRAC, GLOBAL DIGITAL)