×

Wananchi Wakosa Makazi Nyumba Zao Zikibomolewa Kibaha

Zaidi ya Nyumba 200 zilizoko eneo la Mtamba, ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Mji, mkoani Pwani, zinadaiwa kubomolewa na uongozi wa Halmashauri hiyo, kwa madai kuwa wananchi hao wamevamia eneo hilo.

Wakati wananchi hao wakisema hawakupewa taarifa ya ubomoaji huo, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Fokas Bundara amesema ni wavamizi na kwamba walipewa taarifa na taratibu zote zilifuatwa.

Baadhi ya wananchi waliofikwa na changamoto hiyo, wamesema kuwa wanashangazwa na hatua hiyo kwani tayari uongozi wa mkoa ulikuwa katika mchakato wa kuweka utaratibu wa wananchi kugharamia maeneo hayo ili waweze kubaki eneo hilo.

Leave a Comment