×

Heineken Yaendelea Kutangaza Moja Ya Shindano Maarufu Zaidi La Kandanda Ya Vilabu Ulaya-UEFA

Meneja Mkazi wa kampuni ya Heineken Tanzania Ltd, Obabiyi Fagade akiongea na waandishi wa Habari katika hafla ya maonyesho ya fainali ya kombe la UEFA Champions League 2024. Hafla hiyo iliyodhaminiwa na kampuni ya Heineken ilifanyika usiku wa jumamosi katika hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam.

01 Juni, 2024, Dar es Salaam.Wakati Heineken ikiendelea na ushiriki wake wa muda mrefu wa udhamini wa UEFA Champions League unaotarajiwa kuhitimishwa hadi mwisho wa mzunguko wa mashindano ya vilabu 2024-27, mashabiki walikusanyika katika maeneo mbalimbaliya Tanzania kushuhudia mchezo wa fainali kati ya Klabu ya Kihispania Real Madrid na Klabu ya Ujerumani Borussia Dortmund mchezo uliomalizika 2-0 huku timu ya Real Madrid ikiibuka mshindi.

Akizungumza katika moja ya maeneo yaliyoonesha mechi hiyo yaliyoaandaliwa na kampuniya Heineken Beverages jijini Dar es salaam, Meneja wa Kampuni ya Heineken Tanzania Ltd Obabiyi Fagade alisema kuwa mchezo wa mpira na Heineken zina historia ya muda mrefu inayokuza mshikamano, ubora na msisimko.

Kama kampuni iliyo na urithi imara wa muda mrefu katika ulimwengu wa michezo, tuko hapa kupanua ushirikiano wa Heineken-UEFA kwa wateja wetu na mashabiki wa soka nchini Tanzania. Kama mnavyofahamu matoleo ya Heineken ni zaidi ya bia sasa kama tulivyoshuhudia hivi majuzi katika uzinduzi wetu wa biashara mpya ya Heineken kufuatia ununuzi wa Distel ya Africa kusinina Namibia Breweries. Sasa tuna jadala pana zaid ili  na lojumuishamvinyo, Cider na vinywaji vikali ili kukidhi ladha za wateja.

Meneja Masoko wa kampuni ya Heineken Tanzania Ltd, Lilian Pascal akiongea na waandishi wa habari katika hafla ya maonyesho ya fainali ya kombe la UEFA Champions League 2024. Hafla hiyo iliyodhaminiwa na kampuni ya Heineken ilifanyika jumamosi usiku katika hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam.

Mkusanyiko wa leo ni ushuhuda wa ushirikiano kati ya Heineken, Uwekezaji wa kampuni na mchezo wa mpira pamoja na nguvu maalum inayoleta kukusanya watu pamoja na kuunda nyakati za kijamii zisizo sahaulika”.

Katika hafla hiyo, Meneja Masokowa Biashara wa kampuni ya Heineken Tanzania ltd Lilian Pascal, alisema kuwa pamoja na kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu, upanuzi wa biashara yake nchini itanufaisha wateja na jamii ya Tanzania.

“Tumekusanyika hapa leo kushuhudia fainali za Mashindano ya UEFA 2024 kwa hisani ya Heineken ambao ndio

Kutoka Kushoto: Mtangazaji, wa Redio ya Wasafi Maulid Kitenge, DJ Maarufu, DJ Sinorita, Meneja Mkazi wa kampuni ya Heineken Tanzania Ltd, Obabiyi Fagade, Meneja Masoko, wa kampuni ya Heineken Tanzania Ltd, Lilian Pascal wakikwa katika Hafla iliyodhaminiwa na kampuni ya Heineken ilifanyika jumamosi usiku katika hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam.

wadhamini wakuu wa mchezo huo. Biashara Mpya iliyozinduliwa ya Heineken imesaidia kupanua wigo wake na jalada zake nchini Tanzania ambazo zitachangia ukuwaji wa uchumi katika masuala ya ajira, kodi pamoja na wanufaika wengine kama vile wauzaji wa rejareja, wasambazaji na wasafirishaji”.

Kampuni ya Heineken Beverages Pamoja na wageni na wapenzi wa mpira wakitazama tukio la Fainali ya UEFA Champions League iliyodhaminiwa na kampuni ya Heineken katika hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam.

Tukio la utazamaji wa fainali za mashindanoya UEFA 2024 lilifanyika katika maeneo mbalimbali nchini na inafuatia uzinduzi wa hivi karibuni wa chapa mpya za Heineken zinazopatikana nchini Tanzania.

Pamoja na uzinduzi wa biashara mpya na uwekezaji wa kimkakati, Heineken inatoa shukrani zake za dhati kwa wageni wote, washirika, wafuasi na mashabiki wa soka kwa kujumuika katika hafla hii, wakitarajia safari ijayo ya kusisimua.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasilianana:

Lilian Pascal

Heineken- Meneja Masokowa Biashara

+255 744 149 146

[email protected]

Kuhusu Heineken

Heineken ni mojawapo ya kampuni kuu za vinywaji ulimwenguni, iliyojikita kusambaza bidhaa za hali ya juu kwa watumiaji kote ulimwenguni. Kwa uwepo katika masoko 114 pamoja na zaidi ya masoko ya mauzo 180, Heineken inaendelea kupanua jalada lake ili kukidhi mahitaji mbalimbali ya wateja wake.

Leave a Comment