
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), kwa kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) na Wizara zinazohusika na Kilimo Ianzania Bara na Zanzibar na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TENC) wamezindua rasmni kampeni ujulikanyo “KAMPENI YA LISHE zao za Kilishe.
NJIA YA DALADALA”. Ikilenga kuongeza uelewa kwa Wanajamii wote juu ya Mwongozo Wa Taifa wa Chakula na Ulaji Sahihi na kuhamasisha ulaji unaofaa ili kuboresha hali.

*Ziara ya Elimu ya Lishe Bora kwa Njia ya Daladala'” ambayo ndiyo msingi wa Kampeni hii itatumia mbinu ya uhamasishaji wa Afya Bora kupitia uwasilishaji wa ujumbe muhimu wa lishe kwa Umma.
Kampeni hii itatekelezwa katika jiji la Dar es Salaam na Jiji la Mbeya na kwa upande wa Zanzibar itatekelezwa Unguja na itaongezewa wigo kupitia ushirikishaji wa vyombo mbalimbali vya habari ili kwenda sambamba na lengo kuu la kampeni la kuongeza uelewa kwa Wanajamii na kufuata kanuni za lishe bora miongoni mwa Watanzania.
hampeni hii itazingatia Mwongozo wa Taifa wa Chakula na Ulaji Sahihi, ambao unatoa mapendekezo ya kina juu ya matumizi ya mlo kamili kupitia Makundi Sita ya Chakula na umezingatia uwepo wa matumizi sahihi ya vyakula vya asili vilivyopo katika mazingira yetu na kuelekeza vipimo sahihi kwa kila mlo au chakula ambacho binadamu anatakiwa kupata kwa siku.

FAO Tanzania, kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo kwa Ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) kupitia mradi wa AGRICONNEC, inaongoza mradi wa lishe unaoitwa “Kujenga Ustahimilivu wa Mifumo ya Kilimo na Lishe Bora katika Muktadha wa Janga la Kimataifa” Mradi huu umeundwa ili kuongeza uelewa wa lishe bora na kuanzisha mifumo thabiti ili kupunguza changamoto zinaohusiana na janga la upatikanaji wa chakula na soko.
Hivyo Kupitia juhudi hizi za ushirikiano, kampeni ya “LISHE BORA KWA NJIA YA DALADALA” inaenda kuleta matokeo ya kudumu katika ustawi wa lishe ya watu wa Tanzania, kukuza tabia ya ulaji endelevu na yenye afya kwa maisha bora ya baadaye.