×

Zuhura Yunus Na Viongozi Wengine Wazungumza kuhusu Ziara ya Rais Samia Korea – Video

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Juni, 2024 kuhusu Ziara Rasmi ya Kiserikali aliyofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea kuanzia tarehe 31 Mei, 2024 hadi tarehe 05 Juni, 2024.

Mkurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus pamoja na Viongozi wengine wa Serikali wakizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 6, 2024.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji) Mhe. Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar kuhusu masuala ya Uwekezaji wakati wa Ziara Rasmi ya Kiserikali aliyofanya Rais Samia Jamhuri ya Korea.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu masuala mbalimbali ya Teknolojia ya Mawasiliano wakati wa Ziara Rasmi ya Kiserikali aliyofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea kuanzia tarehe 31 Mei, 2024 hadi tarehe 05 Juni, 2024.
 Viongozi mbalimbali pamoja na Waigizaji wakiwa kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari uliofanyika Ikulu Jijini Dar.

 

 

Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano uliofanyika Ikulu Jijini Dar.

Waziri wa Viwanda na Biashara  Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Juni, 2024 kuhusu Ziara Rasmi ya Kiserikali aliyofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea kuanzia tarehe 31 Mei, 2024 hadi tarehe 05 Juni, 2024.

 

Leave a Comment