×

Sherehe Ya Ukuaji Wa Ecobank Tanzania Ulioambatana Na Mafanikio Ya Ecobank Group

Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Dr. Charles Asiedu.

Dar es Salaam, June 2024 – Ecobank Tanzania inayo furaha ya kutangaza ukuaji na mafanikio yake lukuki katika mwaka wa fedha 2023, hii ikiashiria utendaji na uthabiti uliotukuka. Benki hii inatambua kuwa mafanikio haya yametokana na ushirikiano kati ya wateja, wadau na wafanyakazi wake.

Ecobank Tanzania kwa mwaka 2023 imepata mafanikio ya makubwa. Mapato yaliongezeka kwa asilimia 48% na kufikia TZS Bilioni 31.26, kutoka TZS Bilioni 21.11 mwaka 2022. Faida kabla ya kodi (PBT) ikiongezeka kwa asilimia 461% kutoka TZS Bilioni 1.61 mwaka 2022 hadi TZS Bilioni 9.59 mwaka 2023.

Uwiano wa gharama kwa mapato wa Ecobank Tanzania kwa kiasi kikubwa ulikuwa bora Zaidi, ukipungua kutoka 90.56% mwaka 2022 hadi 65.1% mwaka 2023, na hii ikiakisi mikakati madhubuti ya usimamizi wa gharama.Kiwango cha malipo ya mikopo ya malipo ya awali kiliongezeka kwa 79% kutoka TZS bilioni 91.75 mwaka 2022 hadi TZS Bilioni 164.5 mwaka 2023.

Amana za wateja zilipanda kwa 48% kutoka TZS Bilioni 185.97 mwaka 2022 hadi TZS Bilioni 274.59 mwaka 2023, jambo linaloonyesha uhusiano thabiti wa wateja na imani waliyonayo katika huduma za Ecobank. Jumla ya mali iliongezeka kwa 27%, na kufikia TZS Bilioni 406.69 mwaka 2023.

Kwa ubora wa matokeo haya, benki inashikililia nafasi ya juu katika sekta zakibenki na kuongoza kwa kiasi kikubwa katika vipimo muhimu vya sekta. Ecobank Tanzania inashikilia nafasi ya tatu kutoka juu kwa jumla ya asilimia zake za mali kwa 26.7%.

Zaidi ya hapo, ikiwa na 48.33% ya amana za wateja, Ecobank Tanzania imeonekana kuaminika kuhifadhi kiasi kikubwa cha fedha za wateja, huku ikiongoza kwa mikopo na malipo ya awali kwa kiasi cha 79.3%. Vilevile, asilimia ya mapato ya Ecobank Tanzania ya 48.5% inaakisi uzalishaji wake mzuri wa mapato ikilinganishwa na benki zingine. Takwimu hizi zinadhihirisha utawala na ushindani wa Ecobank Tanzania katika sekta ya benki, na hivyo kuimarisha nafasi yake ya kuwa mdau mkuu katika soko.

Hii kasi chanya iliendelea hadi robo ya kwanza ya mwaka 2024, ambapo jumla ya mali iliongezeka kutoka TZS Bilioni 406.69 mwishoni mwa 2023 hadi TZS Bilioni 415.17 kwa mwaka 2024. Zaidi ya hayo idadi ya wafanyakazi iliongezeka kutoka 125 hadi 132, ikionyesha upanuzi wa benki unaondelea na uwekezaji uliofanyika katika rasilimali watu.

Ecobank Tanzania pia imepiga hatua kubwa katika kuboresha uwezo wake kifedha. Uwiano wa mikopo isiyolipika (NPLs) umepungua kwa kasi kutoka 38% mwaka 2020 hadi 2.7% mwaka jana, na hivyo kuthibitisha ukuaji thabiti wa benki hii na usimamizi mzuri wa athari hasi. Benki hii ina matawi matano katika miji ya Dar es Salaam, Arusha na Mwanza, ikiwa na mtandao mpana wa ATM na mawakala zaidi ya 700 nchini kote, ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma zake kwa urahisi.

Mafanikio haya yanawiana na mafanikio mapana ya Ecobank Group, ambayo ni jumuiya ya huduma za kifedha barani Afrika. Licha ya mazingira yaliyokuwa na changamoto kiuendeshaji mwaka 2023, Ecobank Group ililiripoti faida kwenye usawa wa wanahisa wa 24.9% na kuongeza faida kabla ya kodi kwa 8% (au 34% kwa sarafu ya kawaida) na kufikia Dola za Kimarekani Milioni 581. Mapato halisi yalivuka alama ya Dola Bilioni 2 kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2015, yakikua kwa 11% (au 31% kwa sarafu ya kawaida) hadi kufikia Dola za Kimarekani Bilioni 2.1.

Utendaji huu unaangazia mafanikio ya kimkakati ya ukuaji Ecobank Group pamoja na mabadiliko na urejeshaji wake katika kwa kipindi cha miaka mitano (GTR).

Ecobank Tanzania imejitolea kuimarisha huduma zake, kupanua wigo wake na kukuza ushirikiano utakaochochea ukuaji na maendeleo ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania. Benki itaendelea kujitolea kusaidia wafanyabiashara na watu binafsi kufikia malengo yao ya kifedha, na kuimarisha zaidi nafasi yake kama mdau mkuu katika sekta ya benki nchini Tanzania.

Leave a Comment