×

Taharuki Kwa Wakazi Wa Tungutungu Mapinga – Wazimia Baada Ya Nyumba Zao Kupigwa X

WAKAZI wa Tungutungu Kata ya Mapinga Wilaya ya Bagamoyo leo Juni 7, 2024 wamejikuta kwenye taharuki kubwa na wengine wakipoteze fahamu (kuzimia) baada ya nyumba zao kupigwa alama ya ‘X’ Kwa lengo kubomolewa wakidaiwa kuvamia eneo la mtu aitwaye Sevestine Mtunga ambaye ameshinda kesi Mahakama ya Ardhi mjini Kibaha mkoani Pwani.

Wakazi hao wanadai walinunua kihalali viwanja hivyo ambavyo vipo 28 katika eneo hilo likiwa na nyumba na mapagala zaidi 103.

Wananchi hao walifanya jitahada za kumtafuta Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Aboubakar Kunenge na alipofika kwenye eneo la hilo akasema yeye haingilii suala la mahakama ila atajitahidi kuongea na huyo aliyeshinda kesi kuona namna ya kuingia kwenye maridhiano na waathirika wa viwanja hivyo.

Wananchi hao wakati wanasubiria majibu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa leo Juni 7, 2024 wamekuja wawakilishi wa aliyeshinda kesi na dalali wa mahakama pamoja na polisi na kuweka nyumba zote alama ya X zilizopo kwenye eneo hilo tukio ambalo limeibua taharuki kubwa kwa wakazi hao.

Pia wananchi hao wamedai kuwa wameambiwa hadi kufikia Alhamisi ya wiki ijayo kuwa nyumba zote zitakuwa zimebomolewa na mmiliki huyo aliyeshinda kesi.

Leave a Comment