
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameshiriki Mkutano Maalum wa 23 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwa njia ya mtandao Ikulu Dar es Salaam Juni 7, 2024.
Mkutano huo umempitisha Veronica Mueni Nduva (Raia wa Kenya) kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo. Bi. Nduva ni mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo tangu kuanzishwa kwa EAC.
Marais hao wamekubaliana kufanyike Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje na Mawaziri wa Mtangamano kujadili masuala ya amani, ulinzi na usalama pamoja na changamoto zingine zinazoikabili EAC ili kuwasilisha ripoti hiyo kwenye Kikao kijacho cha Wakuu wa Nchi.
