×

Balozi Dkt. Nchimbi Azindua Kiwanda Cha Mwekezaji ‘Tanga Cable’

Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi amesema Chama hicho kitaendelea kusimamia Sera yake itakayohakikisha kuwa Sekta Binafsi inawekewa Mazingira mazuri ya Uwezeshaji katika Suala zima la Uwekezaji hasa kwenye Viwanda vinavyoanzishwa na Wazawa hapa nchini.
Nchimbi ametoa kauli hiyo leo Juni 08, 2024 Jijini Tanga wakati akizindua Kiwanda cha Nyaya za Umeme ‘Tanga Cables’, ambapo amesema ni Muhimu kwa Sekta Binafsi kushiriki katika Ujenzi wa Taifa kupitia Sekta ya Viwanda.
Kwa Upande wake Mkuu wa mkoa wa Tanga Dkt Batilda Burian akizungumza kwenye Uzinduzi huo, amesema Kupitia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 ni kuhakikisha Viwanda vilivyobinafsishwa vinakwenda Kufufuliwa.

Leave a Comment