Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amemrejeshea eneo lake mama mmoja aliyejulikana kwa jina la mama Mugurusi lililopo maeneo ya Tegeta baada ya kuhangaika kwa muda wa miaka 40.
Waziri Silaa amefikia maamuzi hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kuhusu eneo hilo lenye mgogoro huo wa muda mrefu na kufika eneo la tukio kwa kusikiliza pande zote mbili.