
Dar es Salaam, Tanzania – 14 Juni 2024 –Wafanyakazi nchini Tanzania walipata fursa ya kipekee ya kupumzika siku ya Alhamisi, tarehe 13 Juni 2024 jioni, wakati kampuni ya kimataifa ya vinywaji, Heineken, ilipozindua sherehe yake maarufu ya kimataifa, ‘Afterwork By Heineken’, katika kituo cha Samaki Samaki Masaki, Tanzania.
Samaki Samaki, Masaki ambayo ni sehemu maarufu kwa chakula chake cha kipekee pamoja na mandhari manzuri iliburudisha wageni waalikwa kutoka sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na watendaji wa kampuni za biashara, watu maarufu, wabunifu wa vyombo vya habari vya kidijitali na wamiliki wa kampuni mbalimbali, ambao walipata fursa ya kufurahia mchanganyiko wa watu ya kipekee wa kujenga uhusiano na burudani ambayo Heineken inajulikana nayo ulimwenguni.

‘Afterwork By Heineken’imeundwa kutoa mazingira ya kuvutia na ya kufurahisha kwa wafanyakazi kupumzika na kuungana pamoja baada ya siku ya kazi iliyojaa shughuli, huku ikiwapa fursa ya kuungana na wengine.
Katika jamii ya leo, kuwa na nguvu kazi yenye afya na motisha kunahusiana sana na dhana ya uwiano kati ya kazi na maisha, ambayo ni muhimu kwa kukuza nguvu kazi na taifa lenye mafanikio.

Obabiyi Fagade, Meneja Mkaziwa Heineken Beverages Tanzania alisema, “Tunayo furaha kuwaletea ‘Afterwork By Heineken’ kwa wateja wetu wa muhimu nchini Tanzania na tumevutiwa sana na mafanikio ya tukio letu la kwanza hapa.

‘Afterwork By Heineken’imeundwa kuleta mazoea ya kipekee kabisa ambapo wateja wetu wanaweza kufurahia kila kinywaji na kuthamini ujazo uliopo katika kila chupa. Idadi ya watu na hamasa tuliyoshuhudia Samaki Samaki Masaki ilikuwa ya kushangaza. Heineken ina nuru la kuwaleta watu pamoja, na tunafurahi kuwa tunajenga fursa mpya za kuimarisha umoja.”
Wageni walipata fursa ya kufurahia usiku wenye muziki wa moja kwa moja, vitafunwa vyenye ladha nzuri, na aina mbalimbali za vinywaji kutoka kwenye jalada mpya ya Heineken.
‘Afterwork By Heineken’inakuja baada ya uzinduzi wa hivi karibuni wa jalada mpya ya Heineken Beverages nchini Tanzania. Mafanikio ya tukio hili ni hatua muhimu katika juhudi za Heineken za kuunganisha na wateja nchini Tanzania huku ikiongeza uwepo wake kimataifa na kuongeza utamaduni wa ubunifu na furaha katika masoko mapya.