×

Bocco Akutana na Thank You Simba, Hatakuwa Sehemu ya Kikosi

Mshambuliaji bora wa muda wote ndani ya Ligi Kuu Bara, John Bocco

RASMI mshambuliaji bora wa muda wote ndani ya Ligi Kuu Bara, John Bocco hatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kwa msimu wa 2024/25.
Bocco ni miongoni mwa wachezaji wenye uwezo mkubwa kwenye eneo la ushambuliaji wazawa akiwa anashikilia rekodi ya kufunga mabao zaidi ya 100 kwenye ligi.
Mwishoni mwa msimu Bocco aliwashukuru mashabiki na viongozi wa Simba kwa kubainisha kuwa anawashukuru kwa yote kabla ya taarifa rasmi kutoka Simba kumuaga nyota huyo.
Anakuwa ni mchezaji wa kwanza kukutana na Thank You kutoka Simba ambayo itashiriki Kombe la Shirikisho msimu wa 2024/25.
Taarifa kutoka Simba imeeleza namna hii:” Nahodha wetu na mshambuliaji kinara John Bocco hatokuwa sehemu ya kikosi.”

Stori na Lunyamadzo Mlyuka, GPL

#PART2: ANAYEDAI KUNUNUA KIWANJA cha MAMA ANAYELALA NJE MIAKA 11 – ”NAJUTA BABA YAO AMEFARIKI”.

Leave a Comment