
Dar es Salaam 28 Juni 2024: Washindi wa wiki ya tano ya Kampeni ya Zigo la Euro Na Hisense inayoendeshwa na Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo wamekabidhiwa zawadi zao huku mshindi wa tiketi ya kwenda nchini Ujerumani kuangalia fainali za kombe la Euro mwaka huu akikabidhiwa tiketi yake.
Akizungumza kwenye hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi hao, Meneja Biashara wa Kampuni ya Tigo, Fabian Felician amesema washindi hao wamejishindia zawadi mbalimbali kutoka kampuni ya vifaa vya kisasa vya majumbani ya Hisense ambavyo ni luninga ya kisasa (Smart Tv) na friji ya kisasa.

Meneja huyo amesema pamoja na zawadi hizo kuna washindi wengine wa shilingi milioni moja moja ambao na wote walikabidhiwa pesa zao taslimu kwenye hafla hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya Ofisi za Tigo jijini Dar.
Meneja Fabian amesema washindi wa vifaa hivyo vya Hisense na pesa taslimu washijishindia kwa kufanya miamala kwa kutumia App ya Tigo ya Super App huku mshindi wa tiketi akiondoka na ushindi huo kwa kubeti na Pari Mach. Alimalizia kwa kuwataka watumiaji wengine wa simu kutumia mtandao wa Tigo na kutumia Tigo Super App ili waweze kujisogeza kwenye nafasi za kushinda na wao kwani kampeni hiyo bado inaendelea.

Nao washindi hao wakizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi zao waliishukuru kampuni ya Tigo kwa kuendesha kampeni hiyo kiuminifu na kuwafanya washinde zawadi hizo bila kutarajia na hata awali walipopigiwa simu kuelezwa juu ya ushindi wao hawakuweza kuamini kiurahisi mwisho wa siku ukweli ukawa ndiyo huo.