
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa ameingilia kati sakata la kiwanja no. 141/40 kilichopo Ananasifu Kinondoni jijini Dar Es Salaam kilichoachwa na marehemu Abrahamu Isac Mdamo baada baada ya kutokea sintofahamu ya kiwanja hicho kudaiwa mkopo na benki ya NMB kiasi cha shilingi milioni 200 uliochukukiwa na Bwana Michael Mwanda ambaye alikuwa mtu wa karibu na marehemu inadaiwa alifoji nyaraka na kuchukulia mkopo katika benki hiyo na baadae msimamizi wa mirathi Bi. Zainabu Bungire kuitwa benki kwa ajili ya kutakiwa kurejesha mkopo huo.
Aidha Waziri Silaa baada ya kuona taarifa hiyo kupitia vyimbo vya habari alipitia nyaraka na kumuita ofsini kwake jijini Dar Es Salaam msimamizi wa mirathi ya kiwanja hicho ambaye ni Bi. Zainabu Bungire (Mke wa marehemu Abrahamu Isac) na kumtaka amuachie ili aliwasilishe kwa jeshi la polisi walifatilie kwakuwa kuna baadhi ya nyaraka ikiwemo cheti cha kifo kutofautina na nyaraka za murathi hivyo kuhitaji uchunguzi wa jeshi la polisi.