Mwenyekiti CCM Kibiti ataka umoja na ushirikiano kuelekea uchanguzi serikali za mitaa 2024.

Ndondo Cup Shafih Dauda amesema kuwa kwa mwaka huu, mashindano hayo yatachezwa wilayani hapo na atashirikiana na CCM wilaya kuhakikisha kuwa wanatumia hiyo fursa kuhamashisha ushiriki wa uchaguzi wa serikali ya mitaa 2024 pamoja na kutengeneza mafanikio ya chama kwa miaka mitano iliyopita.

‘Michezo kwa sasa ni Ajira, lakini pia ni moja kati ya michezo ambayo inapendwa sana hapa nchini kwetu. Kwa mwaka huu, watu wa Kibiti tunawaletea burundani ya Ndondo Cup na naomba kutoa wito huu mjitokeze kwa wingi kwani pia mtaweza kufahamu ni kwa namna ngani CCM imeweza kuwaletea mafanikio na pia malengo yao kwenye kuelekea uchanguzi wa serikali za mitaa’, alisema Dauda.

Wilaya ya Kibiti inaundwa na kata 16 ambazo zote kwa sasa zinaongozwa na madiwani wa CCM. Kati hizo ni Bungu, Kibiti, Mjawa, Maparoni, Kiongoroni, Dimani, Mtawanya, Mlanzi, Salale, Msala, Mbuchi, Mahege, Mtunda, Mchukwi, Ruaruke na Mwambao.