Mike Mwakatundu ‘Mike Tee’
Stori: Mwandishi Wetu, Risasi Jumamosi
MSANII mkongwe wa Muziki wa Kizazi Kipya, Mike Mwakatundu ambaye ni maarufu kama Mike Tee, amesema mfumo wa uuzaji muziki online umemfanya aridhike na kuamua kurejea tena ulingoni kwani hapo awali kulikuwa na wizi upande wa wasambazaji wa kazi zao.
Akizungumza na gazeti hili kuhusu singo yake ya Kiduchu inayofanya vizuri sokoni hivi sasa, alisema imepokelewa vizuri na mashabiki tofauti na alivyofikiria kwani watu wamependa staili yake aliyochanganya ‘old school’ na ‘new school’.
“Muziki wa sasa pia inabidi ufanye ukiwa na staili tofauti kama tulivyokuwa zamani, yaani kila mtu alikuwa ana staili yake, ukimsikia Juma Nature, Prof Jay, Jay Moe kila mtu alikuwa ana staili yake, muziki wa sasa unakufa haraka kwa sababu wasanii wengi wanaigana staili na melodi,” alisema Mike Tee.