
Waziri wa maji Jumaa Aweso amemsimamisha kazi Meneja wa DAWASA Kibamba anaye julikana kwa jina la Elizabeth Sankere, kutokana na kukosekana kwa huduma ya maji katika eneo hilo changamoto iliyodumu kwa muda mrefu.
“Eliza umefanya kazi kwa muda mrefu hapa kwahiyo mimi nikiondoka naomba tuondoke pamoja, sasa mimi niombe kwakuwa katibu mkuu wetu wa Wizara ya Maji ni mama naomba hii kazi usimamie mwenyewe katibu mkuu” Aweso
Ametoa uamuzi huo Julai 2 wakati wa ziara yake Jijini Dar es salaam katika mtaa wa Malamba mawili, kata ya Kibamba wilayani Ubungo baada ya Wananchi wa eneo hilo kutoa malalamiko kwa meneja huyo aliehudumu eneo hilo kwa kipindi cha miaka minne kuhusu adha ya maji wanayoipata.