×

Azam Fc Yanasa saini ya kiungo mshambuliaji wa Mali

Kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Mali, Cheickna Diakite

Klabu ya Azam Fc imethibitisha kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Mali, Cheickna Diakite, waliyemnunua kutoka miamba ya huko kwao, Real Bamako kwa mkataba wa miaka mitatu.

“Nyota huyo chipukizi, 19, aliyepachikwa jina la staa wa Real Madrid, Mbappe kutokana na kasi na uwezo wake wa kuipenya safu ya ulinzi ya timu pinzani, amesaini mkataba wa miaka mitatu utakaomfanya kudumu ndani viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2027.” imeeleza taarifa ya Wanalambalamba hao.

 

Leave a Comment