
NYOTA Awesu Awesu aliyekuwa ndani ya KMC rasmi Julai 17 ametambulishwa ndani ya Simba kuelekea msimu wa 2024/25 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Nyota huyo alikuwa na mkataba na KMC jambo ambalo liliongeza mvutano kwa mabosi wa KMC na Simba katika kuvunja mkataba wake.
Rasmi Simba wamemtambulisha Awesu kuwa ingizo jipya ndani ya timu hiyo iliyoweka kambi Misri.