×

Mziray ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF

Rais Samia amemteua Shedrack Salmin Mziray kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), awali alikuwa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani (TASAF)

Taarifa ya TASAF imeeleza uteuzi huo ulianza Julai 3, 2024 licha ya taarifa kutolewa jana Julai 18, 2024 na kuwa Mziray alianza kukaimu nafasi aliyoteuliwa Julai 1, 2023 baada ya kustaafu kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji, Ladislaus Joseph Mwamanga

Moja ya changamoto atakazokutana nazo ni malalamiko kuhusu Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini wa TASAF ambao umekuwa ukilalamikiwa na Wadau wa JamiiForums.com kuwa utaratibu sio mzuri na hauwanufaishi walengwa.

GUMZO KADA ALIYEHAMIA CCM ANAFUNGUKA /MAPYA KESI ya MALISA /MAKALA AMTAJA MBOWE | FRONT PAGE

Leave a Comment