×

Kamala Harris Aanza Kampeni Kwenda Ikulu ya White House – Video

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris.

Kamala Harris ameanza siku yake ya kwanza ya kampeni katika kinyang’anyiro cha kwenda Ikulu ya White House huku akiahidi kushinda Uchaguzi wa Urais wa Novemba.

Makamu huyo wa Rais wa Marekani na mgombea anayetazamiwa wa Chama cha Democratic alitoa matamshi hayo kupitia mtandao wa X siku moja baada ya Rais Joe Biden kutangaza kwamba anajiondoa katika kinyang’anyiro cha 2024 na kumuunga mkono mgombea wake huyo.

Bi. Harris alisema atatembelea wafanyakazi katika makao makuu ya kampeni zao huko Delaware.

Aliandika: “Ni siku ya kwanza kamili ya kampeni yetu, kwa hivyo nitaelekea Wilmington, DE baadaye ili kuongea na wafanyakazi wetu kwenye makao makuu.

“Siku moja imepita. Zimebaki 105. Pamoja, tutashinda hili.”-Aliandika Mwana Mama Kamala Harris.

Leave a Comment