×

Alikiba Kukinukisha Tamasha la Simba Day Uwanja wa Mkapa

Msanii nguli wa mziki wa kizazi kipya (Bongo fleva), Alikiba.

MENEJA wa habari wa Simba, Ahmed Ally leo Julai 24, 2024 amemtambulisha msanii nguli wa mziki wa kizazi kipya (Bongo fleva), Alikiba kuwa mtumbuizaji Mkuu wa Tamasha la Simba Day litakalofanyika Agosti 3, 2024 katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Ahmed Ally amesema mbali na Alikiba Kiba burudani zitakuwa nyingi  na wasanii mbalimbali watakaofanya shoo wataendelea kutangazwa kuanzia leo hadi siku ya Simba Day.

Pia Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali amesema miongoni mwa mambo ambayo anatamani kuona ni Simba kuamia Mkoa wa Morogoro na uwanja mkubwa na wenye hadhi ya kimataifa.

Dalali amesema hayo katika stendi ya zamani mjini humo muda mfupi baada ya msafara wa Simba kuwasili ukitokea Dar es Salaam kwa ajili ya kuzindua wiki ya Simba Day ikiwa ni pamoja na kutambulisha jezi za msimu ujao wa 2024/25 kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.

Mwanzilishi huyo wa Simba Day amesema Morogoro timu yao iliwahi kutangaza ubingwa mara mbili wakati akiwa kiongozi, hivyo ina historia nzuri na mkoa huo.

UBAYA UBWELA KIBU ATOROSHWA SIMBA YATOA TAMKO ZITO-YANGA YAAPA KUWAMALIZA TX GALAXY LEO

 

Leave a Comment