
Mjasiriamali na msanii wa filamu za Bongo, Rose Alphonce maarufu Munalove amejifungua mtoto mwingine wa kiume baada ya kupitia maumivu na kejeli nyingi kufuatia kumpoteza mtoto wake aitwaye Patrick, ambaye alifariki Julai 3,2018.
Muna Love ame-share picha akiwa na mtoto wake mchanga wakiwa Hospitali nchini Canada na kuacha andiko lililowagusa wengi huku akiomba ulinzi kwa mtoto wake na kumkabidhi mikononi mwa Yesu. Pia, anawaombea wale wenye uhitaji na waliokata tamaa, wakijazwa imani kama yeye alivyojazwa.
Mwisho, anamtaja Patrick na kumshukuru Yesu kwa kumpa mtoto wakiume tena, ambaye anaitwa “Testimony” na jina lingine la Kiislamu ambalo atalitaja baadae.
“Asante YESU kwanirudishia zaidi ya kile ulichochukua, nikisema nianze kuelezea Matendo yako Makuu juu yangu sitamaliza . Walinipiga fimbo nyingi za maumivu 🥹maneno ya kejeli na kila walichoona nastahili
Lakini sikuchoka Neno langu lilikua wakati nalia kwa uchungu ndani ikiwa mbele zao najikaza najifanya siumii nilikua nakuambia kwa uchungu wewe YESU unajua ukweli unanijua niponye 🥹 Wewe YESU unaona naomba tu niponye uchungu huu 🥹🥹 haya maneno leo najivunia 🙌🏻. YESU ASANTE 🙏
Nilikuahidi kua ukinipa mtoto yoyote tena nikakuomba arudi tu kama yulee atafanya kazi yako kwa Dini zote na nitakutangaza kama chizi nitasimulia Matendo yako Makuu bila aibu nitajivunia wewe popote na hata sasa UMEJIBU MAKUBALIANO YETU . YESU ASANTE 🙌🏻
YESU kama ulivyonipa nakuomba unajua kukutangaza wewe ni vita namfunika mwanangu kwa Damu yako Takatifu atakemgusa au kumnenea mabaya akakutane na wewe Mimi siwezi siwezi zuia chochote Baba yangu ile ahadi niliyokuahidi Ntafanya apa apa walikonikejeli na kunichapa fimbo za maneno nitawaonyesha Ukuu wako najua unaona YESU ila ulinzi wako Baba kwakua sehemu ni hii YESU NAMKABIDHI @testimony_cd TESTMONY MIKONONI MWAKO 🙏
YESU kakumbuke wale wahitaji waliokata tamaa na waliosubiri kwa muda mrefu.
si kama mimi umenipendelea hapana bali wajaze IMANI kama ulivyonijaza na uwajibu kwa kuwapa uzao au kile wanachoomba na kustahili, ili waone Matendo Makuu juu yako
PATRICK naimani umefurahi nisamehe kwakukulaumu ni Uchungu na maumivu makali. YESU ASANTE KWA KUNIPA BABY BOY TENA
Kwakua Maisha yangu na hii Baraka imekuja kama majibu ya maombi yangu basi ataitwa (TESTMONY ) na JINA LINGINE LA MUSLIM NASUBIR NTASEMA 🙏🙌🏻❤️
YESU AKUTUNZE BABA YANGU @testimony_cd 🙏ukue tufanye kazi ya Bwana nakutabiria BARAKA ,FURAHA , HUYU YESU AKUJAZE HEKIMA YA HUDUMA UKATANGAZE NENO LAKE” amesema , Rose Alphonce maarufu Munalove
