
Mama wa marehemu Lucy Haule ambaye inaelezwa kuwa ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kwenye moyo na mwanume aliyekuwa na uhusiano naye wa kimapenzi, amesema kuwa siku ya tukio mwanaume huyo alifika nyumbani kwake na kumuomba aende kuwaona wazazi wake watambuane ili taratibu za ndoa zifuate.

Akizungumza kwa uchungu, mama huyo amesema hakujua kama ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kwa mtoto wake, kwani alimwambia kuwa yeye kama mzazi wa kike hawezi kwenda kwa wa wazazi wa mwanaume bali inabidi wao ndio waje na alivyomwambia hivyo akaondoka.