×

#Exclusive: Binti Mtanzania Anayezungusha Biashara Hadi Afrika Kusini Afunguka Msoto Hadi Kutoboa – Video

Mrembo Vicky Daniel

Mrembo Vicky Daniel ambaye amepata dili kubwa la kuendesha duka lenye bidhaa zote kutoka kampuni kubwa ya vipodozi ya nchini Afrika Kusini, Portia, @portiam_tz hapo jana ameudhihirishia umma kuwa kila kitu kinawezekana chini ya jua baada ya kupata fursa ya kuwa wakala wa pekee wa kampuni hiyo inayouza vipodozi mbalimbali hapa nchini.

Akizungumza na Global TV, Vicky alisema kuwa alianza kuwa na ndoto hiyo akiwa chuoni na baada ya muda akaanza kutumia mafuta kutoka kwa kampuni hiyo ambapo kila mtu alikuwa akimuuliza anatumia nini kutokana na mwonekano mzuri wa ngozi yake ambapo alianza kuagiza kidogo kidogo na kuwauzia wanachuo wengine mpaka alipoweza kutimiza malengo ya kuagiza mzigo mkubwa na hivyo kampuni hiyo kumuamini na kumpa uwakala mkubwa hapa nchini licha ya umri wake mdogo.

Leave a Comment