
Mwigizaji Connie Chiume (72) amefariki Dunia akiwa anapatiwa Matibabu katika Hospitali moja Jijini Johannesburg
Enzi za Uhai wake Connie aliigiza katika vipindi kadhaa vya televisheni vya Afrika Kusini vikiwemo Rhythm City, Zone 14, na hivi karibuni, Gomora
Katika Filamu ya Black Panther ya Mwaka 2018, Connie aliigiza kama Zawavari – Mwanachama wa Baraza la Wakanda. Katika mwendelezo wa filamu hiyo wa mwaka 2022, Black Panther: Wakanda Forever, alichukua nafasi ya Zuri (Forest Whitaker) kama Kiongozi Mzee wa Wakanda.