×

Rais Samia Aweka Jiwe la Msingi Kiwanda cha Kuunganisha Matrekta Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi kwenye kiwanda cha kwanza cha uunganishaji wa matrekta katika ukanda wa Afrika Mashariki leo katika maonesho Kimataifa ya Kilimo ya nane nane 2024 Jijini Dodoma.

Kiwanda hiki cha uunganishaji matrekta kinajengwa kwa ushirikiano kati ya kampuni ya Kitanzania ya Agricom Africa Ltd na Mahindra ya Nchini India kampuni kubwa duniani kwa uzalishaji wa Matrekta.

Kiwanda hiki kipya kitatengeneza matrekta maarufu ya Mahindra yenye nguvu na uimara aina ya Swaraj, chapa inayotambulika na kuaminika kwa miongoni mwa wakulima wa Tanzania.

Itakumbukwa wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara ya Kitaifa nchini India mwezi Oktoba 2023, aliialika kampuni ya Mahindra kuanzisha kiwanda cha uunganishaji matrekta nchini Tanzania.

Kiwanda kipya cha uunganishaji matrekta kinatarajiwa kukamilika mwaka 2025, na kinatarajiwa kuzalisha matrekta 10,000 katika miaka 5 ijayo, mbali na Tanzania kiwanda hiki kipya kitahudumia pia nchi jirani za Afrika, kikiimarisha kujitegemea katika uunganishaji na usambazaji wa matrekta katika ukanda huu.

Kampuni ya Agricom Africa Ilianzishwa mwaka 2009, ikiwa ni msambazaji mkuu wa vifaa vya kilimo nchini Tanzania yenye mtandao mkubwa zaidi wa usambazaji kwenye nchi za Afrika Mashariki.

Leave a Comment