
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo amewaasa Wananchi wa Buchosa kushiriki vyema katika Mkutano wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. Emmanuel Nchimbi utakaofanyika katika Kata ya Nyehunge Agosti 14, 2024 Buchosa, Mwanza.

Ikumbukwe kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi ataambatana na timu yake ambapo mara baada ya kutoka Buchosa wanatarajiwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, Agosti 15, 2024 kuanzia majira ya saa 4:00 asubuhi.


