×

Adaiwa Kumteka Mtoto Wa Miaka 7 Na Kutaka Kumbaka, Amtishia Kisu – Video

Kijana mmoja ambaye hajafahamika kwa jina amenusurika kuuawa Agosti 25, 2024 katika mtaa wa Nyambwela wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam mara baada ya kudaiwa kutaka kumbaka Mtoto (7) (Jina linahifadhiwa) na kumtishia kuwa alitaka kumchoma kisu.

Moja kati ya mashuhuda aliyefahamika kwa jina la Mzee Rashidi Shomali alipata nafasi ya kuzungumza na Global TV na kueleza namna ya tukio lilivyokuwa baada ya kumkamata anayedaiwa kuhusika na tukio hilo.

Lakini pia, Mzee Rashidi ameongezea kwa kueleza kuwa Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kumkamata kijana anayedaiwa kutaka kutekeleza tukio hilo.

Leave a Comment