
MASTAA wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids leo Agosti 28 2024 wanawasili kambini kwa maandalizi ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Al Hilal.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC, Mwenge Agosti 31 ikiwa ni kujipima nguvu kwa timu hiyo ambayo itapeperusha bendera ya Tanzania kimataifa katika kombe la Shirikisho Afrika.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa maandalizi ya mchezo huo yapo vizuri na mashabiki watashuhudia burudani kutoka kwa wachezaji wao.
“Maandalizi ya mchezo wetu wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Al Hilal yapo sawa na wachezaji wataingia kambini Agosti 28 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu huo ambao utachezwa Agosti 31 Uwanja wa KMC, Mwenge.
“Viingilio kwenye mchezo huo mzunguko ni 10,000 na 20,000 kwa VIP, imani yetu ni kwamba tumeweka viingilio sahihi kwenye mchezo wetu huu wa kirafiki dhidi ya Al Hilal ya Sudan.”