×

Harris atetea utendakazi wa White House katika mahojiano ya kwanza

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris alitetea mabadiliko yake ya sera, Rais Joe Biden, na muda wake katika Ikulu ya White House katika mahojiano yake ya kwanza tangu kuwa mgombea wa chama cha Democratic.

Bi Harris alisema kuwa utawala wa Biden uliweza “kuokoa uchumi” baada ya janga hilo na umepunguza uhamiaji haramu katika miezi ya hivi karibuni.

Aliziita sera za Ikulu ya Marekani “mafanikio”, akiashiria kupungua kwa gharama za dawa na kiwango cha ukosefu wa ajira: “Hiyo ni hatua nzuri. Kuna nafasi ya kufanya vizuri zaidi.”

Bi Harris alionekana kwenye mahojiano yaliyorekodiwa ya CNN na mgombea mwenza wake, Gavana wa Minnesota Tim Walz. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kama kufanya mahojiano ya aina hiyo kama mgombea urais.

Makamu huyo wa rais alilazimika kutetea rekodi ya uchumi ya Ikulu ya Marekani, huku mfumuko wa bei na gharama ya juu ya maisha ikiendelea kuumiza vichwa Wamarekani.

Kura za maoni zimependekeza mara kwa mara kwamba wapiga kura wangependelea mgombea wa Republican Donald Trump kushughulikia suala la uchumi.

Lakini majibizano makali zaidi kati ya Bi Harris na mwandishi wa CNN Dana Bash yalijikita katika madai kwamba nafasi za sera za mgombeaji huyo wa Demokratic “zimebadilika” wakati akiwa makamu wa rais na sasa kama mgombeaji wa urais.

EXCLUSIVE: TAJIIRI CHUI AMPA MAKAVU CHIEF GODLOVE -“TAFUTA PESA TAJIRI HAONGEI SANA” -HOTPOT

Leave a Comment