YUSUPH Dabo, Kocha Mkuu wa Azam FC ameweka wazi kuwa wachezaji wapya kwenye kikosi hicho bado hawajaingia kwenye mfumo jambo linalowafanya wachelewe kupata matokeo mazuri.
Azam FC ilicheza mchezo wa kwanza wa ligi Agost 28 2024 dhidi ya JKT Tanzania baada ya dakika 90 ubao ulisoma JKT Tanzania 0-0 Azam FC wakigawana pointi mojamoja.
Dabo amesema: “Ulikuwa ni mchezo mgumu na wenye ushindani, wachezaji wanazidi kuingia kwenye mfumo lakini wengine bado tunapambana kufanya vizuri na tunaamini kwenye mechi zijazo tutapata matokeo chanya.”
Katika mchezo huo Azam FC ilipata kona ya kwanza dakika ya 56 na mpigaji alikuwa ni Idd Suleman, wengi hupenda kumuita Nado.
Stori na Lunyamadizo Mlyuka | GPL