×

Marekani yaikamata ndege ya Rais Maduro wa Venezuela

Marekani imekamata ndege ya Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, ikidai ilinunuliwa kinyume cha sheria kwa kiasi cha $13m (£9.8m) na kutoroshwa nje ya nchi.

Kulingana na wizara ya sheria ya Marekani, ndege hiyo aina ya Falcon 900EX ilikamatwa katika Jamhuri ya Dominika na kuhamishiwa jimbo la Florida nchini Marekani.

Haijulikani ni jinsi gani na lini ndege hiyo iliishia katika Jamhuri ya Dominika. Data ya ufuatiliaji ilionesha ikiondoka kwenye uwanja wa ndege wa La Isabela karibu na mji mkuu Santo Domingo siku ya Jumatatu, na kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Fort Lauderdale huko Florida baadaye.

Venezuela imeshutumu unyakuzi huo, ikisema kuwa ni sawa na kitendo cha uharamia.

Katika taarifa, serikali ya Venezuela ilisema inahifadhi haki ya kuchukua hatua zozote za kisheria kurekebisha uharibifu huu kwa taifa.

Maafisa wa Marekani walisema ndege hiyo ilikamatwa kwa tuhuma za ukiukaji wa udhibiti wa mauzo ya nje na sheria za vikwazo vya Marekani.

Waliongeza kuwa uchunguzi uligundua kuwa watu wanaohusishwa na Bw Maduro walidaiwa kutumia kampuni ya shell ya Caribbean kuficha kuhusika kwao katika ununuzi haramu wa ndege hiyo kutoka kwa kampuni iliyoko Florida mwishoni mwa 2022 na mapema 2023.

Ndege hiyo kisha ilisafirishwa kinyume cha sheria kutoka Marekani hadi Venezuela kupitia Karibiani mwezi Aprili 2023.

Hoja ya maafisa wa Marekani kwamba mauzo ya ndege hiyo ni kinyume na vikwazo vya Marekani haiwezi kuwa na uzito mkubwa kwa Rais Maduro, ambaye mara kwa mara amekuwa akiishutumu Marekani kwa kuingilia masuala ya ndani ya nchi yake.

AJIRA 351 TAWA ZAZUA MTITI BUNGENI – WABUNGE WAKATAA VIGEZO – UWE na MIAKA 25 TU – WACHARUKA

Leave a Comment